Biashara Kiganjani
Simamia biashara yako kwa urahisi . mauzo, hifadhi, madeni, ripoti na zaidi.
About Biashara Kiganjani
Biashara Kiganjani ni programu ya kusimamia biashara ndogo na za kati kwa urahisi kupitia simu yako. Imejengwa kwa ajili ya wafanyabiashara wa Tanzania wanaotaka kufuatilia mauzo, hifadhi, madeni, na matumizi yao kwa njia rahisi na ya kisasa.
Rekodi Mauzo
Hifadhi mauzo yako ya kila siku kwa haraka. Chagua bidhaa au huduma, weka kiasi kilicholipwa, na uhifadhi rekodi. Unaweza pia kurekodi mauzo ambapo mteja amelipa sehemu au hajachukua bidhaa bado.
Simamia Hifadhi
Ongeza bidhaa na huduma kwenye mfumo wako. Fuatilia idadi ya bidhaa zilizopo, pata tahadhari bidhaa zinapopungua, na simamia stoo zaidi ya moja kwa wakati mmoja.
Fuatilia Madeni
Angalia madeni yote ya wateja wako sehemu moja. Rekodi malipo ya sehemu, angalia salio lililobaki, na deni linaondolewa moja kwa moja mteja akimaliza kulipa.
Bidhaa Hazijachukuliwa
Fuatilia bidhaa ambazo wateja wamelipa lakini hawajazichukua. Pata ukumbusho wa kufuatilia ili hakuna bidhaa inayopotea.
Ripoti za Biashara
Pata muhtasari wa biashara yako — mauzo ya kila siku, wiki, au mwezi. Angalia faida halisi, malipo yanayosubiri, na mwenendo wa biashara yako kwa mtazamo mmoja.
Wateja
Hifadhi taarifa za wateja wako ikiwa ni pamoja na majina, namba za simu, na historia ya manunuzi yao. Wasiliana nao moja kwa moja kutoka kwenye programu.
Matumizi ya Biashara
Rekodi matumizi yako kama vile kodi, umeme, mishahara, na gharama nyingine ili upate picha kamili ya faida na hasara za biashara yako.
Fanya Kazi Bila Mtandao
Rekodi mauzo na matumizi hata bila internet. Data yako inasawazishwa moja kwa moja unapopata mtandao tena.
Usalama wa Data
Data yako yote imehifadhiwa kwa usalama kwenye seva za cloud. Unaweza kuingia kwenye akaunti yako kutoka simu yoyote na kupata taarifa zako zote.
Biashara Kiganjani imejengwa na Softsamic Company kwa lengo la kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kusimamia biashara zao kwa ufanisi zaidi.
Similar Apps
Yopal-me
Discover Tanzania like never before.
Nivishe - Ai Photo Editor
Create stunning photo edits by typing, uploading photos, or blending styles.
Nikonekt - Fans & Influencers
Connect with influencers for personalised video messages, promotions, and more.