This is a guide to Knowledge of Islamic Religion Education EDK for the third form
Lengo Kuu la Somo
Somo limekusudiwa kuwapatia Elimu na Ujuzi sahihi juu ya Uislamu wasomi na kuwaandaa kuwa waumini wa kweli watakaoweza kukiendea kila kipengele cha maisha yao ya kibinfsi, kifamilia na kijamii kwa kufuata vilivyo mwongozo wa Qur’an na Sunnah.
Lengo la NUKUU ZA SOMO
Lengo kuu la kuandaa na kutoa kitabu hiki cha NUKUU ZA SOMO ni kuwarahisishia Waalimu na Wanafunzi Kidato cha Tatu kufundisha na kujifunza vizuri somo hili na kuweza kujiandaa vyema katika kuandaa na kufanya mitihani yao ya kati nay a mwisho.
NUKUU ZA SOMO zitatumika kama mwongozo baada ya Mwalimu na Mwanafunzi kusoma kwa kina kitabu cha kiada cha somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu, Kitabu cha Tatu kwa ajili kuandaa vitini vya kufundishia au kujiandaa kwa ajili ya mitihani.
Muundo wa NUKUU ZA SOMO.
Kitabu hiki kimejumuisha mada zilizokusudiwa kumuwezesha mwanafunzi na msomaji mwingine kupata maarifa na ujuzi uliokusudiwa. Mada zilizoandaliwa humo zimetokana na fani kuu tano katika Kitabu cha 2 cha kiada cha somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu, Shule za Sekondari ambazo ni;
Tawhiid
Fiqh
Qur’an
Sunnah na Hadith
Tarekh
Mada zote kuu na ndogo zimeandaliwa kwa kuzingatia na kufuata vyema MUHTASARI WA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU SHULE ZA SEKONDARI KIDATO CHA I - IV, 2012. Hivyo wanafunzi wa Kidato cha Tatu na Wanataaluma wengine wanatarajiwa kunufaika na mwongozo huu.
Kila Mada kuu imetolewa Zoezi la kufanya kama njia mojawapo ya kufanya tathmini ya uelewa wa wasomaji juu ya yale waliyosoma na utekelezaji wake.
Ujuzi wa Somo la E.D.K. Kidato Cha Tatu
Baada ya kumaliza Kidato cha Tatu, mwanafunzi anatarajiwa kuwa na ujuzi wa;
Kutambua vigezo vya kuonyesha kuwa Uislamu ndio dini sahihi.
Kuthibitisha nguzo ya kwanza ya imani hadi ya tano.
Kueleza aina za shirki na kina cha uovu wa shirki
Kupambanua falsafa ya nguzo za Uislamu.
1. Kutambua haki na uadilifu katika Uislamu.
2. Kueleza jinsi Qur’an ilivyohifadhiwa wakati wa Uthman (r.a).
3. Kuthibithisha kuwa Qur’an ni kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w).
4. Kutumia mafunzo ya sura zilizochaguliwa.
5. Kutumia mafunzo ya Hadith zilizoteuliwa kwa mafunzo maalum.
6. Kutambua uanzishwaji na uendeshwaji wa Dola ya Kiislamu Madinah wakati wa Mtume (s.a.w).
Utaweza kujifunza kuhusu mafunzo ya tehama na teknolojia nyingine kama kutengeneza graphics,...
Zijuwe chamsha bobgo ili uweze kuimarisha akili yako. Chemsha bongo zitafanya akili...
Huu ni mkusanyiko wa Hadithi ambazo kwa pamoja zimewekwa katika vitabu vitatu....
Hapa utakwenda kujifunza historia za Mitume 25 waliotajwa kwenye Quran. Utakwenda kujifunza...
Hapa utajifunza kuhusu ibada za kiislamu na utekelezaji wake. Utaweza kujifunza vipengele...
Hizi ni Drsa za dini ya kiislamu. Katika darsa hiziutakwenda kujifunza kuhusu...
Created with AppPage.net
Similar Apps - visible in preview.