Back to Top
Biblia Takatifu - Swahili Bible (Kiswahili) Screenshot 0
Biblia Takatifu - Swahili Bible (Kiswahili) Screenshot 1
Biblia Takatifu - Swahili Bible (Kiswahili) Screenshot 2
Biblia Takatifu - Swahili Bible (Kiswahili) Screenshot 3
Free website generator for mobile apps; privacy policy, app-ads.txt support and more... AppPage.net

About Biblia Takatifu - Swahili Bible (Kiswahili)

Biblia Takatifu ya Kiswahili (Swahili Bible) Agano la Kale na Jipya

Biblia ya Kikristo ni mkusanyo wa maandiko matakatifu ya Ukristo. Maandiko hayo mbalimbali yanaitwa tangu zamani sana "vitabu" tu, inavyomaanishwa na neno "biblia" ambalo ni uwingi wa neno la Kigiriki "biblos" yaani "kitabu".

Hutofautishwa na Tanakh ambayo ndiyo maandiko matakatifu ya dini ya Uyahudi na ambayo pengine inatajwa kwa jina lilelile la "Biblia", hasa katika matoleo ya Biblia ya Kiebrania . Vitabu vyake vimo katika sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo kwa jina la "Agano la Kale".

Biblia ya Kikristo hugawiwa sehemu mbili ambayo ni Agano la Kale na Agano Jipya. Agano la Kale lina maandiko yaliyoandikwa kabla ya Yesu Kristo na vitabu vya Agano Jipya viliandikwa baada yake.

Agano la Kale
Kimsingi vitabu vya Agano la Kale ni vilevile vya Biblia ya Kiebrania, ingawa madhehebu ya Kikristo hutofautiana kidogo katika hilo. Ni kwamba wakati wa kutokea kwa Ukristo palikuwa na tofauti ndani ya Uyahudi kuhusu vitabu vilivyohesabiwa kuwa maandiko matakatifu. Suala hilo liliondolewa kuanzia mwaka 80 BK wataalamu wa Wayahudi wa huko Jabneh (Jamnia) walipochukua msimamo mkali dhidi ya wafuasi wa Yesu.
Kwa wakati huo Wakristo walikuwa wamezoea tayari toleo la Kigiriki la maandiko matakatifu yaliyotafsiriwa katika karne ya 2 KK ambalo linajulikana kwa jina la Septuaginta na kuwa na vitabu kadhaa visivyokuwa vimetunzwa katika lugha asili ya Kiebrania wala ya Kiaramu, au vilivyoandikwa moja kwa moja katika lugha ya Kigiriki.
Hivyo Biblia ya Kikristo ilikuwa na vitabu 7 (viwili vya Wamakabayo, Yoshua bin Sira, Hekima, Tobiti, Yudith na Baruku, pamoja na sehemu za Esta na Danieli) visivyokubaliwa baadaye na Wayahudi.

Vitabu hivyo 7 vikaja kukataliwa na Martin Luther katika karne ya 16, halafu na Waprotestanti wengi, lakini vinazidi kutumiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kwa jina la Deuterokanoni.

Agano Jipya
Kuna vitabu 27 vya Agano Jipya. Vinne vya kwanza ni Injili nne zinazoleta habari za maisha, matendo na maneno ya Yesu.
Vingine ni Matendo ya Mitume, Nyaraka za Mitume, hasa Mtume Paulo, na Ufunuo wa Yohane.

Similar Apps

Daily Bible for Women Offline

Daily Bible for Women Offline

4.8

This Womens Bible app was beautifully designed specially for you Dear Ladies...

KJV Bible, King James Version

KJV Bible, King James Version

4.8

Bible KJV - Offline and free Red Letter edition of the timeless...

Bible Concordance & Strongs

Bible Concordance & Strongs

4.8

King James Study Bible Offline with Strong's Numbers, Bible Concordance and Strong's...

Morning and Evening Devotional

Morning and Evening Devotional

4.8

Daily Reading with C.H. Spurgeon - Morning and Evening DevotionalsIn this app...

Lost Books of the Bible

Lost Books of the Bible

4.8

The Lost Books of the Bible by Rutherford H. Platt, Jr., 1926with...

Bible Study with Concordance

Bible Study with Concordance

4.8

All tools you need for Bible Study for Free in one Offline...

Frequently Asked Questions(FAQ)

Ni nini maana ya Biblia Takatifu ya Kiswahili?

Biblia Takatifu ya Kiswahili ni tafsiri ya maandiko matakatifu ya Ukristo (Agano la Kale na Jipya) kwa lugha ya Kiswahili.

Ni vitabu gani vinavyounda Agano la Kale?

Agano la Kale lina vitabu vya maandiko yaliyoandikwa kabla ya Yesu Kristo. Vitabu hivyo ni vilevile vya Biblia ya Kiebrania ingawa madhehebu ya Kikristo hutofautiana kidogo katika hilo.

Kuna tofauti gani kati ya Tanakh na Biblia ya Kikristo?

Tanakh ndiyo maandiko matakatifu ya dini ya Uyahudi na inatajwa kwa jina lilelile la "Biblia", hasa katika matoleo ya Biblia ya Kiebrania. Vitabu vyake vimo katika sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo kwa jina la "Agano la Kale".

Kuna vitabu vingapi katika Agano Jipya?

Kuna vitabu 27 katika Agano Jipya. Vinne vya kwanza ni Injili nne zinazoleta habari za maisha, matendo na maneno ya Yesu. Vingine ni Matendo ya Mitume, Nyaraka za Mitume, hasa Mtume Paulo, na Ufunuo wa Yohane.

Kuna vitabu gani visivyokubaliwa na Wayahudi na wengine lakini hutumiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi?

Kuna vitabu 7 ambavyo Wayahudi hawakuvikubali na vilikataliwa na Martin Luther na Waprotestanti wengi katika karne ya 16. Vitabu hivyo ni viwili vya Wamakabayo, Yoshua bin Sira, Hekima, Tobiti, Yudith na Baruku, pamoja na sehemu za Esta na Danieli. Hata hivyo, vitabu hivyo bado vinatumika na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kwa jina la Deuterokanoni.
author
AMEN
bahati bahati
author
You are good
Grace Gamba
author
Good
karol Junior
author
Its gòod
Jovinus Matemu
author
Simple to use
Stephano Mlungwana
author
Wonderful!
Morris Mwangata