Back to Top
Herufi na Akili – Akili and Me Screenshot 0
Herufi na Akili – Akili and Me Screenshot 1
Herufi na Akili – Akili and Me Screenshot 2
Herufi na Akili – Akili and Me Screenshot 3
Free website generator for mobile apps; privacy policy, app-ads.txt support and more... AppPage.net

About Herufi na Akili – Akili and Me

Sasa shule zimeanza rasmi. Je, wayajua maendeleo ya mwanao? Umemwandaa kufanya vizuri mwaka huu?

App yetu ya “Herufi na Akili” itampatia mwanao msingi imara wa Elimu!

App hii ni tafsiri ya Kiswahili ya #Akili's Alphabet: Game #1 ya Elimu Tanzania yenye mashabiki wengi, liyopakuliwa zaidi ya mara 10,000 kwenye Play Store!

“Herufi na Akili” inamwandaa mtoto wako kwa ajili ya kwenda SHULE. App hii hutumia michezo na nyimbo kufundisha mwanao jinsi ya kutamka herufi na kumfunza maneno mapya!

Mtoto wako atafurahia ELIMU na app hii ya BURE inayoletwa kwako na waandaaji wa katuni murua ya elimu-burudani ya “Akili and Me.”!

Mwanao atajifunza na Happy Hippo, Bush Baby na Little Lion, akiimba na kusikiliza nyimbo za herufi azipendazo kutoka kwenye kipindi cha "Akili and Me."

Hebu mwone anavyocheza kwa raha, akifurahi na marafiki huku akisikiliza HERUFI zinavyotamkwa na kuzifananisha kwenye simu!

Ubongo, ambao pia ni waandaaji wa katuni nyingine maarufu ya “Ubongo Kids”, wameitengeneza app hii kwa lengo hasa la kumwezesha mtoto wako:

FAIDA
- Atambue sauti za herufi.
- Afananishe herufi.
- Ajifunze kwa uwezo na kasi yake mwenyewe.
- Acheze kwa uhuru.
- Apende kujifunza.

VILIVYOMO
- Jifunze zaidi ya maneno 80 mapya.
- Cheza kwenye mazingira salama kwa ajili ya mtoto.
- Imebuniwa kwa ajili ya watoto wa miaka 3, 4, 5 na 6.
- Haina maksi wala daraja, hivyo mtoto atajifunza bila hofu.
- Ni BURE kabisa. Hakuna gharama zozote.
- Inafanya kazi BILA MTANDAO.

Ubunifu wa “Herufi na Akili” ni kwa ajili hasa ya watoto, hivyo mwanao ataielewa app hii bila shida na kuanza kuitumia mara moja.

Mwonyeshe jinsi ya kupanga na kuoanisha herufi mara moja au mbili tu, kisha tazama jinsi anavyocheza mwenyewe kwa uhuru kabisa na kwa raha zake!

Wangoja nini? Ipakue sasa BURE!

KIINGEREZA - AKILI'S ALPHABET
Ahsante kwa kupakua Herufi na Akili. Tumekuandalia pia tafsiri ya app hii inayoitwa "Akili's Alphabet" inayomfundisha mwanao sauti za herufi na maneno mapya kwa lugha ya Kiingereza.

"Akili's Alphabet" itamwezesha mtoto wako ajifunze lugha ya pili, huku akicheza na kusikiliza nyimbo alizozizoea kutoka kwenye kipindi cha "Akili and Me." Tafuta tu "Akili's Alphabet" hapa Google Play, na utaipata mara moja.

KUHUSU “AKILI AND ME”
“Akili and Me” ni katuni murua ya elimu na burudani inayoandaliwa na Ubongo, watengenezaji wa “Ubongo Kids” na programu nyingine nyingi za kujifunza zilizoundwa mahususi kwa ajili ya watoto wa Afrika.

Karibu Lala Land, ulimwengu wa maajabu, ambapo utajifunza na kucheza na Akili! Imba namba! Cheza herufi! Cheka, chora, na jifunze Kiingereza na Kiswahili na Akili.

Njoo ufurahi na Little Lion, Happy Hippo na Bush Baby kila Jumamosi na Jumapili saa 3 asubuhi kupitia TBC1 (Tanzania), na Jumamosi pekee saa 3 asubuhi kupitia Citizen TV (Kenya).

KUHUSU UBONGO
Ubongo ni kampuni ya kijamii ya Tanzania inayoandaa vipindi na katuni mahususi za elimu na burudani kwa ajili ya watoto wa Afrika, ikitumia teknolojia za kidijitali kama redio, simu, televisheni na vitabu vya mtandaoni kuwafikia popote pale walipo.

Mkakati wetu ni kuwafurahisha wana wa Afrika, tukiwafunza ili wapende kujifunza zaidi kwa uwezo na nafasi yao, wakitumia teknolojia walizo nazo. Njoo utazame vipindi maarufu vya “Ubongo Kids” na “Akili and Me” vinavyofikia zaidi ya nyumba milioni 5.1 barani Afrika.

ONGEA NASI
Kama una maswali, maoni, ushauri ama unahitaji msaada wowote, tafadhali zungumza nasi kupitia [email protected]. Twafurahi sana unapotupa maoni yako.

Similar Apps

Akili's Alphabet —Akili and Me

Akili's Alphabet —Akili and Me

4.4

Akili and Me™School's here. We hope your toddler's READY! Have you given...

Read With Akili - What Do You

Read With Akili - What Do You

5.0

WHAT DO YOU LIKE TO DO?Get to know Akili and her friends...

Ubongo - Kids Videos, Sounds a

Ubongo - Kids Videos, Sounds a

0.0

Enjoy fun, educative videos, audios and books from Ubongo kids and Akili...

Read With Akili - So Many Diff

Read With Akili - So Many Diff

4.9

SO MANY DIFFERENT PLACESJoin Akili on an adventure through night and day,...

Herufi na Akili – Akili and Me

Herufi na Akili – Akili and Me

4.2

Sasa shule zimeanza rasmi. Je, wayajua maendeleo ya mwanao? Umemwandaa kufanya vizuri...

Read with Akili - Akili and th

Read with Akili - Akili and th

AKILI AND THE RIVERJoin Akili and her friends in an adventure that’s...

Frequently Asked Questions(FAQ)

Je, App ya Herufi na Akili inapatikana wapi?

App ya Herufi na Akili inapatikana kwenye Google Play.

Ni umri gani ambao app hii imelengwa?

App hii imebuniwa kwa watoto wa umri wa miaka 3, 4, 5 na 6.

Je, ni gharama gani ya kupakua app hii?

App ya Herufi na Akili ni BURE kabisa.

Je, app hii inaweza kutumiwa bila mtandao?

Ndiyo, app hii inafanya kazi bila mtandao.

Je, app hii ina lugha gani zinazotumiwa?

App hii inapatikana kwa lugha ya Kiswahili.

Je, app ya Herufi na Akili inapatikana kwa lugha nyingine?

Ndiyo, app ya Herufi na Akili inapatikana pia kwa lugha ya Kiingereza kupitia app ya "Akili's Alphabet".

Je, app hii inafundisha nini?

App ya Herufi na Akili inamfundisha mtoto wako kutamka herufi na kumfunza maneno mapya kupitia michezo na nyimbo.

Ni vipindi gani vinavyohusiana na app ya Herufi na Akili?

App ya Herufi na Akili inahusiana na kipindi cha "Akili and Me", ambacho kinapatikana kwenye TBC1 (Tanzania) na Citizen TV (Kenya).

Je, kuna gharama yoyote ya kuangalia kipindi cha "Akili and Me"?

Hapana, kuangalia kipindi cha "Akili and Me" hakuhitaji gharama yoyote.

Ni kampuni gani inayoandaa app ya Herufi na Akili?

App ya Herufi na Akili inaandaliwa na Ubongo, kampuni ya kijamii ya Tanzania inayounda vipindi na katuni za elimu na burudani kwa watoto wa Afrika.
author
Nice app but tells me to use Wi-Fi which I don't have l only have data bundles pls change it
Eunice Wanjiru
author
App hii ni nzuri inasaidia watoto wetu kuelewa namba na kuzishika kwa usahihi hata wakienda shule inakiwa sio ngumu kwao kuzisoma herufi kiukweli nasema hawa ubongo kids wametusaidia sana yani tena mno tunaw...
Khadija Juma
author
Very nice app. Now son can learn how to pronounce letters. Even writing also. 5 🌟
Samson Ntarukundo
author
Thanks for your
Zai Abdala
author
LOVE You PR INCE
Gacheru Ngungu