Back to Top
Mazao Hub Screenshot 0
Mazao Hub Screenshot 1
Mazao Hub Screenshot 2
Mazao Hub Screenshot 3
Free website generator for mobile apps; privacy policy, app-ads.txt support and more... AppPage.net

About Mazao Hub

Fikiria una watu wanaosimamia shamba lako kila siku unatuma hela kwaajili ya matumizi ya shamba lakini hujui kinachoendelea kwenye shamba lako Mwisho wa siku unadanganywa na kuibiwa.

Fikiria unaagiza mbolea au dawa iwekwe kwenye shamba lako lakini haitumiki na kuibiwa.

Fikiria umekosa mkopo benki au uwekezaji kwasababu wewe mwenyewe huna uwezo wa kujua nini kinaendelea shambani kwako wala uwezo wa kufuatilia mashamba yako hatua kwa hatua kuanzia gharama, madawa, mbolea yaani kila hatua za kilimo tangu unaposafisha, unapolima, unapopanda, kupalilia, kukuza mpaka kwenye mavuno mpaka kwenye mauzo.

Fikiria tena, benki au mwekezaji anataka kuwekeza kwako lakini hana uwezo wa kujua historia ya kilimo chako na hata kujua uwekezaji wake hatua kwa hatua kupitia mlolongo mzima wa kilimo chako mpaka kuvuna mpaka kuuza.

Wateja wangapi nje na hata ndani ya Tanzania hawanunui Mazao yako kwasababu hawajui wapi umelima, umelimaje na kwa kiwango gani?

Mazao Hub imetengenezwa kutatua Matatizo hayo yote. Mazao Hub ni mfumo wa kusajili wakulima, kusajili wasimamizi wa mashamba, kusajili mashamba mpaka vitongoji vyake, kusajili mazao yote na misimu yote. Na zaidi Mazao Hub inakusaidia kusimamia kilimo hatua kwa hatua kuanzia kuandaa mashamba, kupanda, kupalilia, kukuza, kuvuna mpaka masoko ndani na nje ya Tanzania.

Pakua APP ya Mazao Hub sasa.

Kupitia Mazao Hub naweza kujua field officers wangu kama wameenda shambani ama la kupitia location monitoring. Na kama wameenda shambani naweza kujua kama mbolea imefika shambani kwani akipiga picha na kuingiza kwenye App ya mazao hub nitajua location ya picha hiyo kama ipo ndani ya shamba ama la. Kupitia Mazao Hub naweza kujua maendeleo ya shamba langu hatua kwa hatua kuanzia wiki ya kwanza mpaka msimu wote mpaka mavuno. Naweza kujua kama kuna mahali nilikosea hatua Fulani , nitajua wapi nilikosea nikashindwa kufikia kiwango Fulani cha mavuno.

PAKUA APP ya MAZAO HUB sasa. Ukikwama Wasiliana nasi kwa namba : +255655973248.
[email protected]
Unaweza kutumia kama website hapa pia: www.mazaohub.com

Similar Apps

EMASUITE PMS

EMASUITE PMS

0.0

EMASUITE PMS.It helps you with menu preparation, inventory tracking, and food sales...

Mashujaa

Mashujaa

0.0

Introducing the Mashujaa Business Centre App, your ultimate companion for effortless transaction...

Hopaje

Hopaje

0.0

Hopaje: Distributor Management & Customer Information. Delivering Swahili Water to diverse locations....

EMA  Retail

EMA Retail

0.0

An App to help businesses Manage, track & report on stock...

author
Useful am really interested using this app
Isaya Msongole
author
Now I know the size of land and set the projection of my farming activities
Josephat Adelard