Back to Top
Muislamu Blog Screenshot 0
Muislamu Blog Screenshot 1
Muislamu Blog Screenshot 2
Muislamu Blog Screenshot 3

About Muislamu Blog

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
Ndugu, Waislamu,
Assalam Alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh
Kwanza kabisa hatuna budi kumshukuru Allah (Subhanahu wata'ala) kwa neema Zake zote alizoturuzuku na kutujaalia kuwa miongoni mwa walioikubali haki na kuifuata. Pia tunamtakia Rehma na Amani Mtume wetu Muhammad (rehema na amani za Allah zimshukie) kipenzi chetu Al- Mustafa aliyeteuliwa kuwa Mjumbe, Muonyaji na Mtoa bishara na Rehma kwa viumbe vyote ulimwenguni. Yeye ametumwa na muongozo wa Kitabu cha Quran na mafundisho ya Sunna zake. Na kwa hakika bila ya muongozo huu tungekuwamo katika kiza totoro na maangamio makubwa.
Madhumuni yetu makubwa ni kuhabarisha (news) na kukumbusha (mawaidha,nasiha, maswali na majibu n.k) kuhusu mfumo wa Kiislamu.
sisi tunaosimamia mtandao huu tunakusudia kujadili na kuchambua fikra, qadhia na matokeo mbali mbali ya uchumi, jamii nk. Na kuyatolea ufafanuzi kwa mujibu wa mfumo wetu mtukufu wa Kiislamu.
Kwa hivyo, tunapenda kuwakaribisha na kuwaalika Waislamu wote katika mtandao huu ili kushirikiana nasi kwa kutoa michango yao ya fikra na maoni katika kujadili, kusoma na kuusambaza mtandao huu kwa kila wanaemjua ili kuasisi majadiliano kwa nia safi kwa lengo la kukuza ufahamu wa Waislamu.
Tunamuomba Allaah atupe tawfiq katika kazi yake hii na atuzidishie ufahamu na upambanuzi wa haki katika kuelezea na kufikisha ujumbe wake huu kwa Waumini wote Inshaallah.

TANBIH
Toviti hii haihusiani na Taasisi yeyote wala kundi/Dhehebu lolote tovuti hii inaendeshwa kwa muongozo wa Quran & sunnah utakapoona sehemu yeyote yenye shida usisite kuwasiliana nasi kupitia email yetu [email protected]
Allaah ndie Muweza wa yote na Kwake ndio mategemeo yetu.
Wasalaam.
Ndugu zenu katika Iymaan na Tawhiyd

author
Asanteni sana
Farida Masoud
author
Tumeisubiri kwa kitambo sana shukrani
Ummu Haarith
author
Nice app, easy to get what you want
Abubakary Zombe